Joto la mpambano wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Young Africans dhidi ya Coastal Union limeendelea kupanda huku saa kadhaa zikisalia kabla ya miamba hiyo kushuka kwenye dimba la CCM Mkwakwani, Tanga.

Mashabiki wa soka mjini Tanga na sehemu za karibu na mji huo tayari wameshajisogeza karibu na uwanja wa CCM Mkwakwani kwa ajili ya kushuhudia kipute hicho ambacho kinatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na hitaji la alama tatu muhimu kwa timu zote mbili.

Kocha mkuu wa Young Africans Cedric Kaze anatazamwa kama muhanga kuelekea mchezo huo, kufuatia matokeo ya kikosi chake kwa siku za karibuni ambayo yamekua hayawaridhishi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Kufuatia hali hiyo Kaze amesema bado anakiamini kikosi chake na hana Presha yoyote kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union, ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Kaze amesema mashabiki na wanachama wa Young Africans wana haki ya kulalamika, lakini yeye kama mkuu wa benchi la ufundi anafahamu majukumu yake ni kuhakikisha anawafurahisha baada ya dakika 90.

”Siogopi presha ndani ya Yanga, mimi ni mwalimu na ninatambua kwamba timu kubwa zina presha ndio maana nikakubali kusaini.

“Mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo ila haiwezi yote kuwa kwa haraka na pia najua kwamba wanahitaji kuona ninatwaa ubingwa hilo siwezi kuwaambia zaidi ya kuwataka waje uwanjani kushuhudia burudani,” amesema kocha huyo kutoka nchini Burundi.

Young Africans bado inaendelea kuongoz amsimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa kumiliki alama 49 baada ya kucheza michezo 21, huku Coastal Union ikishika nafasi ya 13 na alama zake ni 23.

Nchimbi na wenzake kuikosa Coastal Union
PICHA: Simba SC wavamia Khartoum usiku