Kocha Mkuu wa Young Africans amesema hajawahi kupangiwa kikosi na viongozi wa klabu hiyo tangu alipowasili klabuni hapo mwaka 2020, kuchukua nafasi ya kocha kutoka nchini Serbia Zlatko Krmpotić.

Kaze amelazimika kuweka wazi suala hilo, kufuatia tetesi nyingi katika soka la Tanzania, ambapo hudai wa kuwa makocha wengi wamekuwa wakipangiwa vikosi vyao na mabosi wa klabu.

Baadhi ya makocha wa kigeni na wazawa wamewahi kukaririwa wakisema ukweli wa sakata hilo, ambalo huwa kizungumkuti pale timu zinapofanya vibaya.

Kocha kaze amesema amekuwa akifanya kazi kwa uhuru mkubwa akishirikiana na wasaidizi wake, bila kuingiliwa na wanapewa ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi, wanachama na mashabiki kwa jumla.

“Sijawahi kutana na jambo hili kote nilikowahi kufundisha na hata Yanga, ila kama limewahi kutokea basi viongozi wala hawana makosa, aliyekubali kupangiwa timu ndiye ana upungufu.”

“Kwa kocha unayejitambua unatakiwa uheshimu kazi yako, ukimwona kocha anakubali kupangiwa timu maana yake ana kasoro kubwa na haiheshimu kazi yake, binafsi hilo halijanikuta na silitarajii,” amesema Kaze.

Kaze amekua kocha wa kipekee katika ukufunzi wa klabu za Ligi Kuu kwa kuendelea na rekodi ya kutopoteza mchezo wa ligi hiyo tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi.

Waziri Kalemani awasimamisha vigogo Tanesco
Kigonya asimulia penati ya Chama