Rapa Kendrick Lamar amemzawadia toleo jipya la gari, shabiki wake ambaye ni mlemavu wakati akiendelea na ziara yake ya ‘Damn’.

Lamar alimzawadia shabiki huyo aliyetajwa kwa jina la Jennifer Phillips anayetumia jina la @msj3nn kwenye mitandao ya kijamii gari hilo ambalo limetengenezwa maalum kwa ajili  ya kumsaidia mlemavu huyo kuliendesha.

Sambamba na zawadi hiyo ya gari, Lamar alimkabidhi jaketi ambalo aliliandika ujumbe mzuri kwa ajili yake, na Phillips akaweka kwenye mitandao ya kijamii.

“Asante kwa kuniunga mkono. Umekuwa unanihamasisha sana. Una nguvu na mawazo chanya. Ni mwema na mzuri. Kwa miaka yote ambayo umekuwa ukinihamasisha, zawadi pekee ndogo zaidi nayoweza kukupatia ni kuhakikisha unaendesha katika hali nzuri jijini!- K. Lamar.


Naye Phillips aliandika ujumbe wa shukurani zake kwa K Dot na uongozi wake kwa msaada mkubwa aliopewa akieleza kuwa wamemgusa moyo wake kwani alichokuwa akikitaka zaidi ni muziki wao mzuri lakini wamempa zaidi ya hicho.

Kubenea amshukia Ndugai, asema kiatu alichovaa hakimtoshi
Lowassa kuburuzwa kortini

Comments

comments