Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Chelsea Kenedy, leo jumanne anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya, baada ya uongozi wa klabu yake kufikia makubaliano ya kumuuza kwa mkopo kwenye klabu ya Newcastle United.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 jana jioni aliwasili St James’ Park, akitokea jijini London tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya mapema hii leo.

Meneja wa Newcastle United Rafa Benitez amependezwa na kiwango cha mchezaji huyo, baada ya kumsajili kwa mkopo mwezi Januari mwaka huu, na alimtumia mara 13 katika kikosi chake na kufunga mabao mawili.

Kenedy tayari alikua ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Chelsea ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya nchini England, lakini aliarifiwa kuhusu dili la kurejea tena Newcastle United, kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu.

Wakati mipango ya Kenedy kurejea Newcastle United ikitarajiwa kukamilishwa hii leo, tayari uongozi wa klabu hiyo umeshakamilisha mpango wa kumsajili Andros Townsend, akitokeza Crystal Palace.

Townsend amerejea klabuni hapo, baada ya kuondoka mwaka 2016 kwa ada ya Pauni milioni 17.

Picha: Mwigulu Nchemba akikabidhi ofisi kwa Kangi Lugola jijini Dodoma
Video: Mtoto wa miaka 2 ajiua kwa risasi ya baba yake

Comments

comments