Ndege ya Kenya, imeweka rekodi kwa kufanya safari yake kwa mara kutoka nchini humo hadi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy ulioko New York, Marekani.

Ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, KQ002, Kenya Airways iliondoka Jumapili usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na kuwasili New York jana.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wengine walikuwa uwanja wa ndege ambapo sherehe za kuzindua safari hiyo ya kwanza kufanywa na ndege ya abiria ya nchi hiyo zilifanyika saa chache kabla ya kuanza safari.

 

Kenya Airways, KQ ilipata ruhusa ya kufanya safari zake kwenda Marekani tangu Septemba mwaka jana, lakini ilikwama kutokana na viwanja vyake kushindwa kukidhi matakwa husika.

Hivi sasa, badala ya kutumia saa 22, abiria watafanikisha safari ya 13713 KM kutoka Nairobi hadi New York kwa saa 15 tu, wakiokoa zaidi ya saa 7.

Katika safari hiyo ya kwanza, abiria 234 walisafiri na ndege hiyo huku abiria 30 wakiwa kwenye daraja la ‘Business Class’.

Bodaboda yenye ‘GPS’ yawakamatisha wezi, wabakaji
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 30, 2018