Tume ya uchaguzi mipaka, (IBEC), imeendelea kutoa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Ugavana, yaliyoanza kutangazwa Agosti 11, 2022 jioni, huku ujumlishwaji wa kura ukiendelea katika vituo vya kujumlisha kura za kaunti kote nchini.

MATOKEO RASMI YALITOTANGAZWA NA IEBC, NI KAMA IFUATAVYO

Kaunti ya Siaya: James Orengo wa ODM ametangazwa kuwa Gavana mteule kwa kura 220,349. Huku akimshinda mbunge wa zamani wa Raireda, Nicholas Gumbo wa UDM, aliyepata 147,558. 

Kaunti ya Nyandarua: Moses Ndirangu amenyakua kiti cha Ugavana wa Nyandarua kwa kura 158, 263, akimpiga chini Francis Kimemia aliibuka wa pili kwa kura 52,187.

Kaunti ya Bungoma: Gavana wa Kwanza Ken Lusaka (FORD-Kenya) amereja  baada ya kupata kura 241,695 na  kumshinda Wycliffe Wangamati kutoka (DAP-K).

Kaunti ya Pokot Magharibi: Simon Kachapin wa UDA amepata  kura 86,476 na kumshinda Gavana aliyemaliza muda wake John Lonyangapuo. 

Kaunti ya Busia: Paul Otuoma wa ODM amepata kura 164,478 kunyakua kiti hicho, huku John Sakwa wa ANC akiibuka wa pili kwa kura 92,144.

Kaunti ya Homa Bay: Gladys Wanga wa ODM ameshinda kiti cha Ugavana wa Homa Bay kwa kura 244,559,  huku Mgombea huru Evans Kidero akipata kura 154,182.

 Kaunti ya Migori: Ochilo Ayacko wa ODM ashinda kiti cha Ugavana wa Migori kwa kura 175,226, huku John Pesa wa DAP-K akishika nafasi ya pili kwa kura 126,171. 

Kaunti ya Nandi : Stephen Kipyego Arap Sang wa UDA ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 237,045 akifuatwa na aliyekuwa Gavana Cleophas Lagat (Huru) aliyepata kura 54,375. 

Kaunti ya Kisumu: Prof. Anyang’ Nyong’o alichaguliwa tena kuwa Gavana wa Kisumu baada ya kupata 319,957, Jack Ranguma wa NDG anashika nafasi ya pili kwa kura 100,600. 

Kaunti ya Uasin Gishu: Jonathan Bii wa UDA ameshinda kiti cha Ugavana wa Uasin Gishu na mgombeaji wa kujitegemea 214,036 huku Zedekiah Bundotich akipata kura 127,013.

Kenya: Vita ya ubunge yakolea Azimio wakiongoza

Kenya: Waangalizi wa uchaguzi wadai kutengwa
Kenya: Mbunge aliyeuwa ajisalimisha