Waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya wameipongeza tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kwa kuendelea kufanya zoezi lake kwa kwa ustadi licha ya kuripotiwa visa vya kushindwa kuwatambua wapiga kura katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

Waangalizi hao ambao ni Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD), Jumuiya ya Madola na Umoja wa Afrika (AU)/Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ujumbe wa waangalizi nchini Kenya pia wamepongeza uimarishwaji wa ulinzi wakati wa zoezi la upigaji kura.

Waliokaa kutoka kushoto: Marais wastaafu Ernest Bai Koroma (Sierra Leone), Jakaya Kikwete (Tanzania) na Mulatu Teshome (Ethiopia). Picha na Jeff Angote I Nation.

Hata hivyo, timu hiyo ilikosa matumizi ya rasilimali za serikali wakati wa kampeni za kisiasa, ikiwemo vifaa vya mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Uchaguzi wa Kenya (KIEMS), ambavyo vilifeli katika vituo kadhaa vya kupigia kura.

Sambamba na mambo mengine, pia katika uchaguzi huo kulikuwepo na idadi ndogo ya wapiga kura, huku ushiriki wa vijana katika maeneo yoke ya uchaguzi ukiwa si wa kuridhisha ikidaiwa umesababishwa na hali ngumu ya maisha.

Fei Toto, Aziz Ki wamtisha Mtemi Ramadhan
Try Again atamba Simba SC kuiangamiza Young Africans Ngao ya Jamii