Tume ya huru ya Uchaguzi na mipaka (IEBC), imesema mfumo wa kuhesabu kura nchini Kenya haujaingiliwa kwa njia yo udukuzi licha ya uwepo wa ukosefu wa subira katika kungoja matokeo ya urais uliofanyika Agosti 9, 2022.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati amesema hakuna uwiano wowote kati ya maneno yanayosemwa kushabihiana na ukweli wa jambo hilo na kwamba Wakenya wanapaswa kuepukana na Habari potofu na kusubiri muda muafaka wa kuyapata matokeo rasmi ya uchaguzi huo.

Baadhi ya Mitandao ya kijamii nchini Kenya, imekumbwa na tuhuma za kutoa matokeo ya kughushi huku ikidaiwa kuwa takwimu zimekuwa zikipishana na kuleta mkanganyiko kwa jamii na kusababisha taharuki kwa baadhi ya maeneo.

Hata hivyo, Baraza la Habari la Kenya liliitisha mkutano wa vyombo vya Habari kuona namna nzuri ya kutoa taarifa kwa jamii itakayosaidia kuwa na kauli moja badala ya kila mtu kujiandikia ripoti yake kitu ambacho kinaweza kuzalisha maswali na kuondoa uaminifu kwa jamii.

Bado vyombo vya Habari nchini humo, vinaonyesha wagombeaji wawili wakuu Raila Odinga na William Ruto wapo katika ushindani mkali na tume ya uchaguzi ya IEBC ndiyo yenye mamlaka ya mwisho pekee inayoweza kutangaza mshindi halali wa Rais atakaye mrithi Uhuru Kenyatta.

Mapema hapo awali, Chebukati alisisitiza kuwa hakuna haja ya kuziogopa tofauti za idadi ya matokeo kutoka kwa vyombo mbalimbali vya Habari, kwa madai kuwa takwimu zitaoana mwishoni.

Gharama upasuaji magojwa ya moyo hazishikiki
MARATHON: DataVison yatarajia kuandaa Tamasha