Jeshi la Ulinzi la Kenya, limempa Kamanda Mkuu, Rais Uhuru Kenyatta mkono wa kwaheri ya kupendeza ambayo ilijazwa na jumbe za utumishi na uzalendo kabla ya kustaafu kwa Mkuu huyo wa Nchi siku ya Jumanne Agosti 13, 2022.

Rais Uhuru Kenyatta avutwa na Maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi toka Makao Makuu ya Idara ya Ulinzi (KDF) wakivuta gari alilopanda Rais Uhuru Kenyattawakati wa hafla ya kumuaga Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya. Picha na Jeff Angote/NMG.

Sherehe kuu ya kumuaga Uhuru Kenyatta, ziliandaliwa na Wanajeshi hao wa Ulinzi kuthamini jukumu lake katika kuboresha na kupanua wigo wa jeshi katika kipindi chake cha miaka 10.

Rais Uhuru ambaye ana uhusiano mazuri na wanajeshi, hakuficha furaha yake ya kukaa nao siku nzima akiandamana na Mkewe Margaret Kenyatta na wanawe wawili.

Kenyatta alisema, “Asanteni sana Mungu awabariki, nitawakumbuka lakini bado tuko pamoja.” aliwaambia askari hao na kuwashukuru kwa utumishi wao wa kujitolea, kwa nchi.

Tukio hilo lilianza kwa Mkuu wa Nchi kufanya ukaguzi wa gwaride la heshima katika uwanja wa Ulinzi ndani ya gari rasmi la Kamanda Mkuu, akiwa na msaidizi wake na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Robert Kibochi huku Makomandoo wa Maroon wakimpa heshima na bendi yake kupiga wimbo anaoupenda wa UB40 unaoitwa Cherry oh Baby.

Wakati wa utawala wa Kenyatta, KDF iliongeza uwepo wa wanajeshi nchini kwa kuinua Kambi ya Manda Bay hadi kambi kamili ya kijeshi na kuzinduliwa kwa Modika Barracks mwaka 2019, ambayo ni kambi ya kwanza ya kijeshi Kaskazini mwa Kenya.

Katika utawala wake, Rais Kenyatta na Serikali walianzisha hospitali ya ngazi ya sita ya vikosi vya ulinzi huko Kabete, ikaboresha Hospitali ya Memorial Defenses, hospitali ya mkoa ya Isiolo, hospitali ya mkoa ya Eldoret na kuanzisha kituo maalum cha afya cha vitanda 80 kwa wanajeshi wanaorejea vitani.

Wafugaji washauriwa kununua ardhi, kufuga kisasa
Polisi watuhumiwa kwa rushwa mpakani