Mvutano umeibuka katika ukumbi wa Bomas of Kenya, wakati wabunge wa Azimio walipomshutumu Mwakilishi wa Wanawake wa Uasin Gishu Gladys Boss Shollei, ambaye ni wakala wa UDA kunakili kisiri fomu za 34B zilizofanyiwa marekebisho kisha kuziingiza kwa siri kwa makarani wa meza ya uthibitishaji ili kutangazwa na IEBC kama matokeo yaliyothibitishwa.

Mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang, ajenti wa Azimio, amesema ana wasiwasi juu ya suala hilo kuw ahuenda linafanyika katika vituo vingi huku mtuhumiwa Bi. Shollei, akikanusha madai hayo kwa kupayuka, “Sijafanya kosa lolote.”

Hata hivyo, makamishna wa IEBC Justus Nyang’aya, Abdi Guliye na Francis Wanderi waliingilia kati kuwatuliza maajenti wa Azimio waliotaka atolewe nje ya ukumbi huo, huku aliyekuwa Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi, Rachel Shebesh pia akiungana na Mbunge wa Azimio mteule Opiyo Wandayi (Ugunja) na TJ Kajwang kumshutumu Bi. Shollei kwa upotofu.

Wakati hayo yakitokea, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hakuwa ndani ya ukumbi huo huku jaribio la Polisi la kutaka kuwaondoa waandishi wa Habari, waangalizi na mawakala katika eneo la ukumbi likishindikana.

Viongozi wanaounga mkono muungano wa Azimio, unaoongozwa na TJ Kajwang wakielezea wasiwasi wao kuhusu zoezi la uhakiki linaloendelea. Picha na Nation Media.

Mpaka sasa mgombea wa UDA, William Ruto anaongoza kwa asilimia chache ambazo ni 49.91 kwa kupata kura 6,703,493 dhidi ya Mgombea wa Azimio Raila Odinga mwenye asilimia 49.41 akiwa na kura 6,636,849 na ujumlishaji wa matokeo bado unaendelea.

Kenya: Ni vicheko na vilio nafasi za Ugavana
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 13, 2022