Mahakama imesema imeifunga Mahakama ya Sheria ya Milimani jijini Nairobi kwa siku 11 kuanzia Ijumaa Agosti 26, 2022 ili kutoa nafasi ya kusikizwa kwa kesi za uchaguzi wa urais ulifanyika Agosti 9, 2022.

Kituo hicho cha mahakama, kitakuwa mwenyeji wa muda wa vikao vya Mahakama ya Juu wakati wa kusikilizwa kwa maombi tisa ya Urais, yaliyowasilishwa na watu tofauti na mashirika ya kiraia kupinga ushindi wa William Ruto katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

Kesi hiyo, itafanyika katika Ukumbi wa Sherehe wa Mahakama ya Milimani, tofauti na maombi ya awali ambapo kesi hiyo ilifanyika katika Jengo la Mahakama Kuu, ndani ya Wilaya ya Biashara ya Jiji.

Inasemekana kuwa, majaji saba wa mahakama kuu hawatatumia jengo la zamani kwa kukosa nafasi ya kutosha kulingana na kanuni za janga la Uviko-19 huku katika notisi iliyotolewa siku ya jana Jumanne Agosti 24, 2022, Mahakama ikisema katika kipindi cha siku 11, dharura, mambo yatashughulikiwa kwenye majukwaa ya mtandaoni.

“Mawakili wote, mawakili wa upande wa mashtaka, wateja, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, kumbuka kuwa Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Milimani na Mahakama ya Trafiki hazitafikiwa kwa urahisi kutokana na kusikilizwa kwa maombi ya Uchaguzi wa Rais kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 5, 2022 ,” inaonesha ilani hiyo.

“Fahamu zaidi kwamba maombi mapya na cheti cha dharura vitawasilishwa na kushughulikiwa katika Mahakama ya Jiji na mambo yote yaliyopangwa kwa kipindi hiki yatatajwa kwa maelekezo ya mahakama husika katika kipindi hicho,” ilisema taarifa hiyo.

Waombaji wa pingamizi la urais ni pamoja na waliowasilishwa na kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga na mgombea wake Martha Karua, Wanaharakati Okiya Omtatah na Khelef Khalifa, David Kairuki Ngari, Youth Advocacy Africa(YAA), John Njoroge Kamau, Juliah Chege na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rueben Kigame.

Kenya: Odinga atinga Mahakamani ‘kibabe’ na Lori la ushahidi

Zolan Maki achekelea mwaliko wa Sudan
Nandy 'avikwa umalkia' tuzo za Grammy