Mwenyekiti wa United Democratic Alliance (UDA), Johnson Muthama na Ajenti Mkuu wa Chama hicho, Josephat Nanok ni miongoni mwa watu muhimu ambao hawajatajwa katika Baraza la Mawaziri 22 lililotangazwa na Rais William Ruto Septemba 27, 2022.

Nanok, ambaye alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa timu ya kampeni ya urais ya Kenya Kwanza Alliance, alikuwa mtu muhimu katika Sekretarieti ya Dkt. Ruto kama mmoja wa maajenti wakuu wa Kenya Kwanza ambapo wakati wa kampeni, alipewa jukumu la kuwa Mwenyekiti na kuratibu shughuli za vikundi vyote vya kuhakikisha kuna ushirikiano na uwiano.

Katika eneo la Nyanza, aliyekuwa gavana wa Migori Okoth Obado, aliyevumilia wimbi la kinara wa ODM Raila Odinga kwa kuungana na Ruto, pia amekosa nafasi ya Baraza la Mawaziri na alikuwa kiongozi wa Ruto aliterajiwa kwa kiasi kikubwa kuteuliwa kwenye Baraza la Mawaziri.

Mwenyekiti wa United Democratic Alliance (UDA), Johnson Muthama. Picha na Tuko.

Hali hiyo ya kuukosa Uwaziri, pia imewakumba walioharakisha kutia saini mikataba ya baada ya uchaguzi na Dkt Ruto akiwemo Mbunge wa Ugenya, David Ochieng na aliyekuwa Gavana wa Kisii, James Ongwae huku Eliud Owalo, mshirika wa Ruto kutoka eneo hilo akituzwa hati ya mawasiliano, inayotarajiwa kuidhinishwa na Bunge.

Eneo la Mlima Kenya, Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro alipigiwa upatu kuwa katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri lakini hali imekuwa tofauti baada ya tangazo la baraza hapo jana akiungana na Prof. David Ndii, mtaalamu wa uchumi ambaye alisimamia kampeni za Dkt. Ruto.

Seneta wa Mandera, Ali Roba ambaye pia alitia saini mkataba wa baada ya uchaguzi na Rais Ruto, hakuhusika katika uteuzi huo na sasa inasubiriwa iwapo atapewa kamati ya Seneti kuwa mwenyekiti au nafasi yeyote kati ya wabunge saba waliochaguliwa chini ya chama chake, iwapo atapata nafasi za uongozi wa kamati katika Bunge la Kitaifa.

Josephat Nanok. Picha na Whonskenya.com

Roba, ndiye kiongozi wa chama cha United Democratic Movement (UDM), kilichoshinda nyadhifa mbili za ugavana, viti saba vya ubunge na viti 35 vya Wabunge wa Kaunti katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022 akiungana na Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko, ambaye amekosa nafasi ya Uwaziri.

Sonko, alihama Azimio na kujiunga na Kenya Kwanza akifichua kwamba alikuwa ameahidiwa nyadhifa za kuteuliwa ambapo baadaye (Julai, 2022), alitweet kuhusu mambo mazuri ambayo alikuwa ameahidiwa ikiwa Ruto iwapo atashinda baada ya kukutana na Rais Ruto, (Naibu Rais wakati huo).

Sonko alisema, “Hapa chini kuna nafasi zinazotolewa kwangu na watu wangu kama ilivyoainishwa katika makubaliano ya ushirikiano/MoU: Waziri mmoja, serikali ya kitaifa; PS tatu, serikali ya kitaifa; mabalozi wanne; CEC watatu, Kaunti ya Mombasa; maafisa wakuu watatu, Kaunti ya Mombasa; CECs mbili, Kaunti ya Nairobi; na maafisa wakuu watatu katika Kaunti ya Mombasa, kwa baraka zako, ningetaka kuingia katika mkataba huu na UDA, ili niwe na uhakika wa kazi na fursa kwa watu wangu wa Mombasa na Nairobi.”

Mike Sonko. Picha na Twitter.

Naye, Katoo ole Metito, ambaye aliwania kiti cha ugavana wa Kajiado lakini akashindwa na mgombeaji wa ODM, Joseph ole Lenku, pia amekosa fursa ya kuhudumu katika Baraza la Mawaziri na kuungana na Hassan Omar, ambaye alipoteza kinyang’anyiro cha ugavana wa Mombasa dhidi ya mgombea wa ODM, Abdulswamad Nassir ambapo pia Nicholas Gumbo, ambaye aliwania kiti cha ugavana wa Siaya kwa tiketi ya UDM ya Roba, alitarajiwa pia kuwepo katika Baraza la Mawaziri lakini hali imekuwa tofauti.

Wakili aliyemtishia Bunduki shahidi akutwa amekufa
Ally Kamwe akaribishwa ulingoni Soka la Bongo