Makamishna wanne kati ya saba wa tume huru ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kusema hawayatambui matokeo yaliyotangazwa jana na Mwenyekiti wao Chefula Wabukati.

Makamishna hao waliokuwa mbele ya vyombo vya Habari hii leo Agosti 16, 2022 wamesema upo mkanganyiko katika baadhi ya mahesabu na kudai kuwa kuna matokeo ambayo yalipokelewa na hayakujumlishwa.

“Hatutaki kushiriki hiyo dhambi maana kuna kura hazikujumlishwa na hizo kura zinawez kuleta tofauti au ushindi kwa yeyote na kutokana na sababu hizi hatutambui matokeo yaliyotangazwa na tume ya IEBC hapo jana,”

Naibu mwenyekiti wa IEBC, Juliana Cherera, akiwa na Makamishna Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya ambao kwa pamoja wamedai matokeo ya mwisho yalifikiwa kwa njia isiyoeleweka. Picha na NMG.

Wamesema hakuna ambaye hajui hesabu kwani Chebukati alitangaza kuwa kuna mgombea amepata asilimia 100.2 ya kura kitu ambacho si sahihi na kinaleta mkanganyiko hivyo wameamua kujitokeza na kuelezea hisia zao ili umma utambue ni kwanini walijitenga.

Makamishna hao, ni Naibu mwenyekiti wa IEBC, Juliana Cherera, Makamishna Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya ambao kwa pamoja walidai kuwa matokeo ya mwisho yalifikiwa kwa njia isiyoeleweka, bila kutoa maelezo zaidi.

Takwimu za sensa kusaidia utoaji wa huduma kwa Wananchi
Kenya: Raila akataa matokeo ya urais, asema hatakubali