Kamati ya matayarisho ya utwaaji wa Ofisi ya Rais imefanya kikao chake cha uzinduzi hii leo Agosti 12, 2022 chini ya Mwenyekiti wake Joseph Kinyua ambaye amesema tarehe ya uapisho wa Rais itatangazwa hapo baadaye.

Mwenyekiti huyo wa kamati, ameyasema hayo wakati wa zoezi la muonekano wa eneo la Ikulu atakaposimama Rais mteule wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Harambee House, akisema watakuwa wakifanya masasisho ya mara kwa mara ya mchakato huo.

Amesema, tarehe ya kuapishwa kwa rais mteule itatangazwa kuwa ya mapumziko na kwamba mamlaka ya kamati hiyo yataanzishwa mara tu tume ya uchaguzi itamtangaza rasmi Rais mteule.

Hata hivyo, Kinyua amesema jukumu la kamati hiyo ni kuwezesha mchakato wa kukabidhiana madaraka kati ya Rais anayeondoka madarakani na Rais mteule na kwamba itapanga watu wa usalama, wafanyakazi na vifaa kama itakavyohitajika na Mteule.

Kamati hiyo pia itawezesha utoaji wa taarifa za rais mteule na maafisa mbalimbali wa umma na kuandaa hafla ya kuapishwa kwa rais mteule.

Serikali yamtaka Wakili Mkuu kusimamia majukumu yake
Tahadhari yatolewa uwepo wa mapigano karibu na Nyuklia