Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa ambaye alikuwa akitafutwa na Polisi nchini Kenya kwa tuhuma za mauaji ya msaidizi wa mpinzani wake kisiasa, Brian Olunga hatimaye amejisalimisha.

Mbunge huyo, amejisalimisha katika kituo cha Polisi cha Bungoma baada ya kupewa muda wa kufanya hivyo na Jeshi hilo la Kenya ambapo anadaiwa kumpiga risasi Olunga katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi usiku wa Agosti 9, 2022.

Didmus Barasa wakati wa Kampeni eneo la Eldoret nchini Kenya, mapema mwaka huu 2022. (Picha na Capital News).

Matandao wa Citizen Digital, uliripoti kuwa mpinzani huyo wa kisiasa wa Barasa, Brian Khaemba alifika katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi ili kushuhudia zoezi la kuhesabu kura.

Taarifa hiyo ilisema kulitokea na hali ya kupishana iliyopelekea mauaji hayo na kusababisha Barasa ambaye ametangazwa kushinda kiti cha Ubunge wa eneo hilo kukimbia kusikojulikana hadi alipojisalimisha baada ya tangazo hilo la Polisi kutolewa.

Kenya: Haya hapa matokeo ya Uchaguzi wa Gavana
Maadhimisho ya miaka 50 ya STAMICO