Waziri wa Afya Cleopa Mailu, amesema kuwa kikao kati ya wafanyakazi hao wa Sekta ya Afya kilichopangwa jana jioni kiligomewa na wafanyakazi hao na kuashiria kuanza kwa mgomo wao.
Waziri Mailu amesema kuwa mgomo huo ni batili sababu mahakama ilitoa siku 90 kwa Serikali na vyama hivyo vya wafanyakazi wa sekta ya Afya kufanya mazungumzo na kufikia muafaka, na siku hizo 90 bado hazijakamilika.
Chama cha Madaktari (KMPDU) na kile cha Wauguzi (KNUN) vimesisitiza kuwa havitorudi kazini mpaka madai yao yatakapotimizwa.
Kufuatia mgomo huo, jana takribani wagonjwa wa akili 100waliotoroka kutoka katika hospitali kuu ya magonjwa hayo iliyopo eneo la Mathare jijini Nairobi. Jeshi la Polisi limetangaza kuanza msako wa kuwasaka wagonjwa hao ambao huenda wanaweza wakaleta madhara kwa raia.
Pia mgomo huo umepelekea wagonjwa 2000 waliokuwa wanatakiwa kupatiwa huduma ya upasuaji kutopewa huduma hiyo sababu ya kutoonekana kwa madaktari wa upasuaji.
Madai haya mapya ya Madaktari na Wauguzi kama yakifikiwa, kima cha chini cha mshahara kwa Daktari kitakuwa Shilingi 6,840,000 na Kima cha juu kitafikia 18,800,000.