Naibu afisa mrejeshaji wa kura katika eneo Bunge la Starehe anashikiliwa na vyombo vya usalama baada ya kukosekana kwa masanduku matatu ya kura.

Kukamatwa kwa afisa huyo, kunatokana na Viongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Edwin Sifuna, Philip Kaloki, Reuben Ndolo, Maina Kamanda, Racheal Shebesh na mgombeaji wa ubunge wa Jubilee Starehe Amos Mwago walivamia kituo cha kujumlishia kura kutaka matokeo ya uchaguzi yatolewe.

Viongozi hao, walihusisha masanduku ya kura yaliyokosekana na wizi wa kura katika kitu cha mtuhumiwa cha eneo la Starehe katika Shule ya Upili ya Jamhuri jana Alhamisi Agosti 11, 2022 majira ya jioni.

Wakihutubia wafuasi wao katika Shule ya Upili ya Jamhuri, viongozi hao walitaka maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), katika kituo cha kujumlisha kura wachukuliwe hatua kueleza mazingira ambayo masanduku ya kura yalitoweka.

Mawakala na wafuasi wa wagombea mbalimbali waliodai kuwa kulikuwa na mipango ya kuchakachua chaguzi kwa kuwapendelea baadhi ya wagombea, na kusema mchakato wa kujumlisha kura ulikuwa ukicheleweshwa.

Bw Sifuna alitaka matokeo ya ubunge na Wabunge wa Bunge la Kaunti yatolewe kufikia leo asubuhi, ambapo pia akawataka maafisa wa IEBC kuharakisha shughuli hiyo na kutangaza matokeo ya eneo bunge la rais, seneti na mwakilishi wa wanawake bila kuchelewa zaidi.

“Lazima matokeo yatolewe leo usiku, wafuasi hawataondoka katika kituo hiki hadi wagombeaji walioshinda watangazwe,” alisema Sifuna huku Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Starehe akisema, ” itabidi mtuvumilie na kutupa muda zaidi wa kukamilisha kazi yetu kabla hatujatoa matokeo ya mwisho.”

Hadi kufikia sasa, matokeo ya awali yanaonyesha kuwa mgombeaji wa Jubilee Amos Mwago, anaongoza katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Starehe kwa kura 51,000 akifuatiwa na Simon Mbugua wa United Democratic Alliance ambaye amepata kura 35,000.

Kenya: Mwenyekiti IEBC atishia kuwatimua Mawakala
Serikali yamtaka Wakili Mkuu kusimamia majukumu yake