Ikiwa zimebaki saa chache, ili Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya, baadhi ya wakazi katika maeneo mbalimbali hasa yale ambayo ni ngome za wagombea waliokuwa wakichuana vikali za Raila Odinga na William Ruto, wameanza kusherehekea huku kila mmoja wao akiwa na imani ya kushinda.

Hata hivyo, maandalizi ya utoaji wa matokeo yameendelea kufanyika huku Mwenyekiti wa IEBC, Chefula Wabukati akisisitiza suala la amani na na kukubali matokeo halisi yatakatotangazwa na tume hiyo baadaye hii leo.

Ukumbi wa Bomas nchini Kenya.

Tatari Luninga mbalimbali zimeanza kurusha matangazo ya moja kwa moja huku vikundi vya nyimbo vikiendelea kutumbuiza katika ukumbi ulioandaliwa na IEBC ambayo imesema matokeo ya mwisho yatatoka saa tisa alasiri Agosti 15, 2022.

Kwa upande wa Wagombea wa urais George Wajackoyah wa chama cha Roots na David Mwaure wa chama cha Agano Party, wamewasili katika ukumbi wa Bomas, eneo ambalo zinafanyika shughuli za ujumlishaji wa kura.

Mwisho wa 50 Cent na Mayweather wabainika
Serikali yaidhinisha mgao wa Taulo za kike bure