Naibu Rais William Ruto amenyakua viti vitano kati ya saba vya ugavana katika eneo la North Rift, huku viti vya Trans Nzoia na Turkana vikichukuliwa na Azimio la Umoja One Kenya.

Katika eneo la Turkana, Gavana anayemaliza muda wake, Josphat Nanok ameshindwa kuwasilisha kiti hicho kwa United Democratic Alliance (UDA), huku Jeremiah Lomorukai wa Orange Democratic Movement (ODM), akiambulia kura 66,631 na kumshinda mgombeaji wa UDA John Lodepe Nakara, aliyepata kura 33,639.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri, John Munyes ambaye aligombea kwa tiketi ya Jubilee na kupata kura 41,866 huku Joseph Atol wa Chama cha Mabadiliko akiwa wa mwisho kwa kura 1,352.

DP eneo la Uasin Gishu, baada ya zaidi ya miaka 20 ya kujaribu bahati yake katika siasa za uchaguzi, Jonathan Bii almaarufu kama Koti Moja, alitangazwa mshindi wa kiti cha ugavanawa eneo hilo.

Ushindi wake unatokana na majumuisho ya mawakala baada ya kupata kura 214,036 dhidi ya kura 127,013 za mpinzani wake, Zedekiah Bundotich almaarufu kwa jina la Buzeki ambaye aliwania kiti hicho kama mgombea huru.

Kenya: Luninga zasitisha kutangaza matokeo
Kenya: Madai ya udanganyifu wa matokeo yazidi kutawala