Uwezekano wa kifo na umwagaji damu kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi na woga wa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ulimlazimu kiongozi wa Azimio Raila Odinga, kukubali ushindi wa Rais, William Ruto.

Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition, Raila Odinga, alipoamua kutoa ya moyoni kwa timu yake ya kampeni ya urais, akisimulia ni kwa nini aliamua kuchilia “ushindi wake wa kura” bila kuitisha maandamano.

Kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition, Raila Odinga (katikati) akipeana mkono na Rais William Ruto. Anayepiga makofi kushoto ni Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Picha na Nairobi news.

Kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022 na uamuzi uliofuata wa Mahakama ya Juu uliothibitisha ushindi wa Rais Ruto, Odinga alijitokeza na kuzungumza juu ya sakata hilo lililokwisha.

Odinga pia amesema, wafuasi wake kwa jinsia tofauti walioongoza kampeni yake ya tano ya urais katika harakati zake za kujenga demokrasia, wanapaswa kupongezwa na kwamba Jamii ya Wakenya wasihuzunike na jinsi majaribio yake ya kutwaa nafasi hiyo ya juu kushindikana mara kadhaa.

Ujenzi Jengo la Wizara wafikia asilimia 50
Wahimizwa ubunifu upatikanaji maji safi na salama