Afisa Mkuu wa Polisi, Sabina Kerubo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mwandishi wa Habari wa The Star, Eric Oloo, ambapo mwili wa marehemu ulikutwa nyumbani kwake mnamo Novemba 21.

Afisa huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Siaya, James On’gondo ambaye aliamuru aendelee kuwa kizuizini Kituo cha Polisi cha Siaya kwa siku 14.

Katika hati ya kiapo, wapelelezi wanaoshughulikia kesi hiyo wameomba muda wa nyongeza wa kumshikilia Afisa huyo ili kumaliza uchunguzi juu ya mauaji yaliyo tendeka.

Aidha, wiki mbili zilizopita Mahakama iliamuru ndugu wawili, Victor Ogola Luta na Franklin Joel Luta, kukamatwa kwa uchunguzi zaidi.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa tena mnamo tarehe 10 Desemba mwaka huu.

DC kigamboni atangaza vita watoto kukaa 'vibanda umiza'
Video: Mwakinyo amvaa Mzee Rashid Matumla, amtangazia ‘vita’