Kiongozi wa Muungano wa Azimio La Umoja Raila Odinga anatubia taifa siku moja baada ya Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais huku akiyapinga matokeo hayo.

Bw Chebukati alimtangaza mgombeaji wa Kenya Kwanza William Ruto kuwa Rais Mteule baada ya kupata kura 7,176,141 akimshinda Bw Odinga aliyepata Kura 6,942,930.

Kiongozi huyo wa Azimio, alitoweka katika uwanjani Bomas of Kenya ambapo IEBC ilitangaza matokeo. Katika hali mbaya zaidi, makamishna wanne kati ya saba wa IEBC walikanusha matokeo ya urais muda mfupi kabla ya Chebukati kutangaza mshindi wa kura hiyo iliyokuwa na upinzani mkali.

Makamishna hao, akiwemo naibu mwenyekiti Juliana Cherera, makamishna Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya walidai kuwa matokeo ya mwisho yalifikiwa kwa njia isiyoeleweka, bila kutoa maelezo zaidi.

Kenya: Makamishna waungana na Odinga kukataa matokeo ya Urais
Wanane wafariki katika ajali Mbeya