Matokeo ya Urais nchini Kenya yaliyoanza kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), usiku wa kuamkia leo Agosti 12, 2022 mpaka sasa yanaonesha hakuna tofauti kubwa ya mpishano kati ya Wagombea wawili wanaochuana, Raila Odinga na William Ruto.

Kwa mwaka huu, zoezi la uchaguzi nchini Kenya limekuwa tofauti na nyakati zilizopita kutokana na IEBC, kutotangaza matokeo moja kwa moja kadiri wanavoyapokea na badala yake vyombo vya Habari navyo vimepewa wigo wa kujumlisha matokeo ingawa hitimisho litafanywa na Tume pekee.

Hata hivyo, kumekuwepo kwa hofu miongoni mwa wananchi wanaofuatilia matokeo hayo kutokana na utaratibu uliopo licha ya mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati kuwasihi kuwa na utulivu.

Kenya: Ruth Odinga mwakilishi wa kike Kisumu
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 12, 2022