Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza Baraza la mawaziri, ambapo kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri. 

Prof. Kithure Kindiki ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, huku Hazina ikiongozwa na aliyekuwa gavana wa CBK Prof Njuguna.

Ruto, pia amemteua Aden Duale kuwa Waziri wa Ulinzi, Aisha Jumwa katika Utumishi wa Umma na aliyekuwa Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua kuwa Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora.

Rais wa Kenya William Ruto. Picha na NMG.

Hati ya Ardhi, ikiongozwa na Zachariah Mwangi Njeru, Kilimo na Maendeleo ya Mifugo ni Mithika Linturi na Wizara ya Afya ikiongozwa na Susan Nakhumicha Wafula.

Dkt. Ruto pia amemteua Alice Wahome kuwa Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira, Moses Kuria kuwa Waziri wa Biashara huku Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiongozwa na Rebecca Miano.

Wizara ya Barabara, Uchukuzi na Ujenzi wa Umma, itaongozwa na Kipchumba Murkomen huku Soipan Tuya akiteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mazingira na Misitu.

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi. Picha na K24.

Peninah Malonza, anachukua nafasi ya Najib Balala kama Waziri wa Utalii, huku Eliud Owalo akiteuliwa katika hati ya Mawasiliano. 

Ezekiel Machogu, atachukua nafasi ya George Magoha kama Waziri wa Elimu huku mshirika wa muda mrefu wa Ruto, Davis Chirchir akielekea katika Wizara ya Nishati.

Wizara ya Masuala ya Vijana itaongozwa na Ababu Namwamba, Vyama vya Ushirika na Simon Chelugui, Wizara ys Madini ikiongozwa na Salim Mvurya na Wizara ya Leba itaongozwa na Bi Florence Bore. 

Katibu wa Baraza la Mawaziri, Mercy Wanjau. Picha na Techweez.

Rais Ruto, amesema uteuzi mwingine wa baraza la mawaziri utafuata hivi karibuni, ambapo Katibu wa Baraza la Mawaziri anayemaliza muda wake wa Nishati na Petroli wa Kenya, Bi Monica Juma, sasa anakuwa mshauri wa usalama wa kitaifa. 

Wengine waliopewa nyadhifa Serikalini ni pamoja na Justin Muturi ambaye atakuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, huku Mercy Wanjau akiteuliwa kuhudumu kuwa katibu wa baraza la mawaziri.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 27, 2022
Waziri Mkuu ashiriki mazishi ya Shizo Abe