Wizara ya Afya Kenya imepiga marufuku maduka ya dawa na wakemia kuuza dawa za Chloroquine na Hydroxychloroquine kwa watu wasio na kibali cha kutumia dawa hizo kutoka kwa Daktari.

Agizo hilo linakuja baada ya watu nchini humo kuanza kununua dawa hizo kwa wingi kufuatia madai kuwa zinaweza kutibu corona baada ya visa vya Corona kuongezeka nchini humo.

Ikumbukwe wiki chache zilizopita rais wa Marekani Rais Donald Trump alidai Chloroquine inaweza kuwa tiba ya corona kauli ambayo imepelekea uhitaji mkubwa wa dawa hiyo Marekani na nchi nyingine.

Taarifa iliyotolewa kwa watumishi wote wa afya imesema matumizi mabaya ya madawa hiyo yanaweza kusababisha upofu wa maisha kwa mtumia bila ya kuwa na maelekezo kutoka kwa mtabibu.

Hata hivyo, wataalamu wa afya bado hawajaruhusu vidonge hivyo kutumika kwa ajili ya kutibu Virusi vya Covid 19.

Aliyeua mfanyakazi Arusha apandishwa kizimbani, aongezewa shtaka la Mirungi
CORONA: RFEF kuzisaidia klabu zenye hali mbaya kiuchumi