Shirika la Kuzalisha Umeme nchini Kenya (KenGen) limewaomba radhi wananchi baada ya umeme kukatika kwa takribani saa nne nchi nzima baada ya kuzimwa na ‘tumbili’.

Katika taarifa yao kwa umma, KenGen imeeleza kuwa walimkuta tumbili huyo akiwa katika eneo la ‘swichi’ ya mtambo wa kuzalishia umeme katika eneo la Bwawa Kuu la Gitaru, Mashariki mwa nchi hiyo.

KenGen imesema kuwa huenda tumbili huyo ndiye aliyezima umeme nchi nzima baada ya kuiangukia na kusababisha hitilafu kwenye mashine ndogo yenye megawati 180 na kupelekea tatizo hilo.

“Mitambo ya kuzalisha umeme kote nchini Kenya huwa imezingirwa na nyaya za umeme ilikuwazuia wanyama wa porini kuingia humo na kusababisha madhara kama hayo ya jana,” inasomeka taarifa hiyo na kuongeza kuwa wamechukua hatua ili tatizo hilo lisijirudie.

Tumbili huyo alisalimika na amechukuliwa na shirika la huduma kwa wanyama pori nchini humo kwa ajili ya kupewa huduma ya matibabu.

Abdu Kiba aonesha nia ya kufanya kazi na WCB
Hillary Clinton ajitangazia ushindi, aandika historia Marekani