Katika matokeo ambayo tayari yametangazwa yanaonesha wagombea wa Azimio la Umoja wa Raila Odinga wana Wameshinda viti 134 na wagombea wa Muungano wa United Democratic Alliance (UDA), wa William Ruto ukiwa na viti 88 ambapo.

Mpaka kufikia sasa matokeo yanaonesha UDA ya Dkt Ruto inaongoza kwa kura chache, lakini Odinga anaongoza katika viti vya ubunge, huku utangazaji wa matokeo ya ujumla ukiwa bado unakwenda taratibu.

Hata hivyo, vita vya Bunge ni kubwa kwani itatoa mwelekeo wa nani ana nguvu sana Serikalini kwa kuwa na idadi kubwa ya Wabunge huku hamu ya wengi ni kutaka kujua nani ataibuka kumrithi Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta.

Kushinda urais bila kudhibiti Bunge itakua ni habari nyingine kwani yaweza pelekea baadhi ya maamuzi ikiwemo upitishaji wa sheria na miradi kukwama, kutokana na uwingi wa wabunge wanaotofautiana vyama na Rais aliye madarakani.

Vita ya Ubunge, pia inataka ushindi wa kura kwa theluthi mbili ambayo itaruhusu chama au muungano wa vyama kupata udhibiti kamili wa Bunge na kuwa na mamlaka ya kuidhinisha au kukataa mapendekezo yenye mabadiliko ya katiba pamoja na udhibiti wa maamuzi muhimu, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha au kukataa kura ya maoni.

Kenya: Wakenya roho juu wakingojea matokeo ya uchaguzi mkuu
Kenya: Ruth Odinga mwakilishi wa kike Kisumu