Wakati wakenya wakiendelea kungoja kwa hamu matokeo ya uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi huu, huku mahasimu wawili wanaowania urais wa nchi hiyo wakiwa wanachuana vikali.

Kiongozi mkongwe wa upinzani, Raila Odinga, mwenye umri wa miaka 77, ametupa karata yake kwa mara ya tano akiutaka urais, huku naibu wa Rais William Ruto, mwenye umri wa miaka 55, naye akitupa karata yake ya kuuta urais wa nchi hiyo.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, haijatoa idadi kamili ya matokeo wala haijasema itamtangaza lini mshindi, lakini matokeo yasiyo rasmi na yale yanayotangazwa na vyombo vya habari, yanaonesha kuwa kila mmoja kati ya wawili hao anakaribia asilimia 50.

Kisheria ni IEBC pekee yenye mamlaka ya kutangaza rasmi washindi wa uchaguzi huo, ingawa tume hiyo imetowa madaraka kwa vyama na vyombo vya habari kukusanya matokeo hayo.

Pacha aliyebakia Muhimbili naye afariki
Kenya: Vita ya ubunge yakolea Azimio wakiongoza