Wanasayansi nchini Kenya wameungana na wenzao wa Kimataifa katika juhudi za kutafuta chanjo ya ugonjwa wa Covid -19, kwa kufanyia majaribio dawa tatu.

Majaribio ya chanjo atafanyiwa binadamu ili kubaini ikiwa dawa hizo zinaweza kutibu.

Watafiti hao wametafuta idhini ya kufanyia majaribio dawa aina tatu ikiwa ni pamoja na Remdesivir, ambayo iliidhinishwa na Marekani kama dawa ya dharura, Dawa ya kutibu malaria ya Hydroxychloroquine na Lopinavir/Ritonavir, ambayo pia inatumiwa na wagonjwa wa HIV.

Mtafiti Mkuu katika uchunguzi huo, Dkt. Loice Achieng Ombajo, ambaye ni mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika hospitali ya Kenyatta amesema mpaka sasa hakuna tiba  anayopewa mgonjwa ila wanasaidiwa kukabiliana na dalili zinazoonekana kama vile homa kali na vidonda vya koo.

Dkt. Ombajo ameongeza kuwa katika majaribio ya tiba, wagonjwa wengi wanashirikishwa bila mpangilio maalumu lakini wote wanapewa dawa tofauti hivyo bado hawajabaini ni dawa ipi inafanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Corona: Serikali yaendelea kushughulikia changamoto zinazojitokeza mipakani
Azam FC: Tuna changamoto, lakini tutapambana