Mahakama ya Juu nchini Keny,a itaamua iwapo mgombeaji urais William Ruto na mgombea mwenza wake Rigathi Gachagua watatwaa mamlaka baada ya kukubali kusikiza ombi la wanaharakati 11 waliotaka kuzuia kuapishwa kwa Ruto na Bw Gachagua iwapo tume ya uchaguzi itawatangaza washindi wa uchaguzi wa urais.

Kesi hiyo, imeitishwa na naibu msajili wa mahakama ya upeo Bernard Kasavuli, alisema faili hiyo itawekwa mbele ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, kwa ajili ya uteuzi wa benchi ya majaji watano kubaini ombi la wanaharakati hao, ambapo Ruto na mgombea mwenza wake, wanapambana ili kufuta kesi hiyo.

Bw Kasavuli amesema, “Wahusika katika kesi hiyo baadaye watafahamishwa kuhusu ombi lao baada ya uamuzi wa mahakama na faili hiyo itawasilishwa mbele ya Naibu Jaji Mkuu kwa ajili ya kuunganishwa na benchi ya kusikiliza na kuamua ombi hilo kwa rekodi. Pande zitafahamishwa uamuzi huo utakapotolewa.”

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), chini ya mwenyekiti wake Wafula Chebukati, katika jibu la pamoja kwa kesi hiyo walisema mahakama ya upeo, haina mamlaka ya kushughulikia masuala yaliyoibuliwa na wanaharakati, kuhusu kustahiki kwa tiketi ya Ruto na Gachagua kutokana na masuala ya uadilifu kwa upande wa pili.

DP Ruto, Gachagua na chama chao cha UDA walisema mahakama haina tu mamlaka ya kusikiza kesi hiyo lakini pia kesi hiyo haifai na ina dosari isiyoweza kushughulikiwa hivyo haiwezi kutekelezeka.

Bunge ambalo bado halijateuliwa, pia litasikiliza pingamizi zilizotolewa na tume ya uchaguzi, dhidi ya Gachagua na chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 14, 2022
Serikali yatoa taarifa mwenendo wa Uviko-19