Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC), imesema kwamba katika uchaguzi uliofanyika Agosti 9, wananchi waliojitokeza kupiga kura ni 56.17%, pekee ya waliojisajili maana kuwa zaidi ya wapiga kura milioni 10 walisusia mchakato huo.

Kamishna wa IEBC Francis Wanderi, ametaja jumla ya wapiga kura milioni 22.1 waliojiandikisha walipaswa kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia siku ya Jumanne, Agosti 9.

Ripoti hiyo ya IEBC imesema hadi kufikia saa kumi na moja jioni wakati vituo vya kupiga kura vilipokuwa vikifungwa, takwimu za IEBC zilionyesha kuwa karibu wapiga kura milioni 12 kati ya 22.1 milioni walishiriki zoezi hilo.

Kamishna Wanderi amesema idadi ya wapiga kura waliojitokeza Jumanne, Agosti 9, ilikuwa ya chini zaidi ikilinganishwa na chaguzi za 2013 na 2017 ambapo asilimia 85.9 na 79.5 walishiriki.

Katika eneo la Mlima Kenya linalokusudiwa kuwa na wingi wa kura, kaunti ya Nyeri ndiyo iliandikisha idadi ndogo ya wapiga kura ikilinganishwa na chaguzi za 2013 na 2017.

Hadi kufikia sasa matokeo ya muda yaliyotangazwa na fomu 34A kutoka vituo vya kupigia kura tofauti nchini Kenya yameonyesha kuwa William Ruto amepata zaidi ya kura milioni 1, akifuatwa na mpinzani mkuu Raila Odinga.

Jumla ya wapiga kura milioni 22.1 waliojiandikisha walipaswa kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia Jumanne, Agosti 9.

Romy Jones ampa waraka mzito Diamond
AFRIKA SUPER CUP kuzinduliwa Arusha-Tanzania