Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) limetangaza rasmi kujiondoa kuwa mwenyeji wa michuano ya soka kwa nchi za Afrika mashariki (Cecafa Senior Challenge) kutokana na ukata wa fedha.

Kenya ambao ni mabingwa watetezi waliandaa mashindano hayo kwa mafanikio makubwa mwaka jana 2017 na kuibuka mabingwa.

Raisi wa shirikiso hilo, Nick Mwendwa amesema kuwa waliitarifu bodi ya maandalizi ya mashindano Cecafa kuwa watafute nchi nyingnine itakayo andaa mashindano hayo yanayovuta hisia za mashabiki wengi wa soka Afrika Mashariki.

’’Kenya haitoweza kuandaa mashindano ya Cecafa kutokana na na ukosefu wa fedha’’ amesema Mwendwa.

Aidha, mwishoni mwa wiki iliyopita Kenya pia ilijitoa kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kuchukua nafasi ya kuandaa mashindano ya soka ya maitaifa ya Afrika kwa wanawake (AWCON) baada ya Ghana kushindwa kufanya maandalizi ya mashinano hayo.

Kenya waliandaa mashindano hayo mwaka jana 2017, na kuibuka mabibwa baada ya kuifunga Zanzibar kwenye mchezo wa fainali.

Michuano ya Cecafa Senior Challenge hufanyika kila mwaka na kushirikisha mataifa ya Uganda, Kenya,Tanzania, Rwanda, Burundi, Zanzibar, South Sudan, Sudan, Eritrea, Djibouti, Somalia na Ethiopia.

Ndalichako: Hatutoi mabilioni ya fedha watoto wakapoteze maisha shuleni
Gianni Infantino, Donald Trump wakutana kwa mara ya kwanza