Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wa usalama nchini humo, Bwana Joseph Nkaissery, imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote nchini humo, kufuatia vifo vya watu kadhaa vilivyosababishwa na maandamano ya upinzani ya kutaka tume ya uchaguzi nchini Kenya kufanyiwa mabadiliko.

Bwana Nkaissery, akihutubia mkutano wa wanahabari alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na waandamanaji hao kubeba silaha butu na mawe wakisababisha uharibifu mkubwa na kuhatarisha usalama wa taifa.

Kenya2Kenya

Video: Wanajeshi Chad Kupambana na Boko Haram Niger, 4 Wauawa Katika Shambulizi
Liverpool Wahangaika Na Usajili Wa Mshambuliaji