Mahamaka ya Juu nchini Kenya imezuia kwa muda ndege zinazotoka China kuingia Kenya, uamuzi huo umetolewa katika shauri lililofunguliwa na Chama cha Wanasheria.

Pia, imewazuai Waziri wa Afya, Waziri wa Usafirishaji, Waziri wa Mambo ya Nje, Mwanasheria Mkuu na Mamlaka ya viwanja wa Ndege nchini humo kuruhusu kuingia kwa mtu yeyote kutoka China.

Jaji James Makau aliyetoa hukumu hiyo amesema ni kwa faida kubwa ya Umma. Itakumbukwa pia Rais Kenyatta ameunda Kikosi Maalumu cha kushughulika na mlipuko wa Virusi vya Corona.

Aidha, Waziri wa Afya, Usafirishaji na Mambo ya Nje wameamuriwa kuwatafuta abiria wote 239 waliongia nchini humo wakitokea China Februari 26, 2020.

Pia, Wizara hizo tatu zimetakiwa kuwafuatilia, kuwachunguza na kuwaweka katika uangalizi maalumu katika Kituo cha Jeshi la Ulinzi la Kenya abiria wote 239 walioruhusiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta.

Membe atoa kauli ya kwanza baada ya kufukuzwa CCM
Mafua yamuandama papa Francis

Comments

comments