Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemualika aliyekuwa mpinzani wake mkuu kwenye uchaguzi wa Urais wa August 8 mwaka huu, Raila Odinga kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Ofisi ya Rais, Joseph Kinyua alisema kuwa pamoja na Odinga, wagombea saba walioshiriki uchaguzi wa awali na uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 pia wamealikwa.

Odinga amerejea nchini humo hivi karibuni baada ya kwenda mapumzikoni. Wawakilishi wake walitangaza kuwa atafanya maandamano makubwa katika siku hiyo ya kuapishwa kwa Kenyatta.

NASA wameendelea kushikilia msimamo wao kuwa hawamtambui Kenyatta kama Rais halali wa Kenya, licha ya Mahakama kubariki ushindi wake wa uchaguzi wa marudio ambao Odinga aliususia.

 

Marais takribani 20 wa nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwa ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wamethibitisha kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.

Messi avunja rekodi nyingine, atunukiwa kiatu cha dhahabu
Dkt Slaa ‘amsampraiz’ Profesa Lipumba