Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa haki za mashoga zina umuhimu lakini umuhimu mkubwa uko katika maadili ya wananchi wa Kenya.

Ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la televisheni ya Marekani CNN, ambapo Uhuru amesema kuwa suala hilo halina mjadala na linakwenda kinyume na imani za Wakenya waliowengi.

“Nataka niweke wazi, sitojihusisha na suala ambalo halina umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Kenya. Hili siyo suala la haki za binadamu, hili ni suala la kijamii, lakini ni misingi tu ya utamaduni kama watu bila ya kujali unatokea katika jamii gani,”amesema Uhuru Kenyatta

Amesema kuwa sheria za Kenya zinaweka wazi kuwa ushoga ni kinyume cha sheria na Wakenya waliowengi wanakubaliana na hilo.

Hata hivyo, hii ni mara ya pili Uhuru anazuia mjadala juu ya haki za mashoga baada ya kutupilia mbali wito wa Barrack Obama ukiitaka serikali yake kuwakubali makundi mbalimbali ya mashoga mwaka 2015.

Wabakaji kuhukumiwa kifo nchini India
Video: Jason Darulo, Diamond Platinumz waachia wimbo wa kombe la dunia ''Colours''