Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa ameshangazwa na kitendo cha kujiuzulu kwa Mwanasheria mkuu nchini humo, Githu Muigai.

Muigai aliteuliwa kushika wadhifa wa kuwa mwanasheria mkuu na rais Kenyatta baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2013, na kuchukua nafasi iliyokuwa imeshikiliwa kwa muda mrefu na Amos Wako.

Aidha, Muigai alijichukulia umaarufu mkubwa wakati wa kesi zilizowakumba rais Uhuru Kenyatta na makamu wake, William Ruto kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, mjini The Hague, Uholanzi, ambapo aliwatetea kwa dhati viongozi hao.

Akizungumza muda mfupi baadaye kutoka ikulu ya Nairobi, Kenyatta amesema kuwa amemteua jaji Paul Kihara Kariuki, kuwa mkuu mpya.

Hata hivyo, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu ya kujiuzulu kwa mwanasheria huyo wa nchi hiyo.

Shonza awataka waandishi wa habari kuzingatia maadili
Video: Makonda awakingia kifua bodaboda ''Marufuku kukamata Bodaboda''