Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kukomeshwa kwa mgogoro Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao unachochea mvutano wa Kidiplomasia kati ya DRC na Rwanda.

Kenyatta ambaye ni mpatanishi wa mgogoro huo, amesema ana wasiwasi juu ya hali inayozidi kuwa mbaya katika eneo la Kivu Kaskazini, ambako mapigano makali yamekuwa yakiripotiwa kati ya makundi yaliojihami kwa silaha, wanajeshi wa serikali na M23.

Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, witi huu wa Kenyatta unakuja ikiwa ni siku moja baada ya Rwanda kuishambulia ndege ya kivita ya Congo kwa madai ya kukiuka sheria na kuingia katika anga yake.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alisema ndege ya kivita aina ya Sukhoi 25 kutoka Congo, iliingia katika anga yake kwa mara ya tatu kupitia eneo la Rubavu karibu na mji wa Goma, na hatua za kujilinda zikachukuliwa.

Rais Samia ateta na wadau Kilimo na Chakula
Tanzania yanufaika miradi mapambano hali ya jangwa