Ziara ya rais wa Marekani nchini Kenya, Barack Obama inayosubiriwa kwa hamu na wakenya imezua tetesi nyingi ikiwa ni pamoja na kuunganisha ziara hiyo na mazungumzo ya kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.

Kufuatia tetesi hizo, leo (Julai 21) rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewatoa wasiwasi wakenya kuhusu suala hilo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya Obama nchini humo. Amesema mazungumzo yao hayatagusa masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambayo ni kinyume cha sheria na tamaduni za nchi hiyo.
“Kama wakenya, taifa letu linakabiliwa na changamoto nyingi tu nafikiri tuna masuala ya muhimu zaidi ya kujadiliwa mbali na hilo la mapenzi ya jinsia moja,” alisema rais Kenyatta.
Rais Obama anatarajia kuanza ziara yake nchini humo siku ya Ijumaa huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa na kikosi maalum cha Marekani kwa kushirikiana na jeshi la Kenya katika kila kona za jiji la Nairobi linalokabiliwa na vitisho vya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabaab.

Lembeli Aeleza Kilichomuondoa CCM Kuhamia Chadema
Marekani Yapinga Uhalali Wa Uchaguzi Wa Burundi, Wawili Wauawa