Ofisi ya Bunge imesema kuwa kesho jumamosi ya Mei 2, 2018 kutakuwa na hafla ya kupokea taarifa za kamati maalumu zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai za kuchunguza na kushauri kuhusu sekta za uvuvi wa bahari kuu na Gesi asilia.

Ambapo Spika wa Bunge atapokea na kukabidhi serikalini taarifa hizo katika hafla itakayofanyika katika viwanja vya Bunge mbele ya lango kuu la kuingilia ukumbi wa Bunge kuanzia saa 3:30 asubuhi.

Hafla hiyo itahudhuriwa na wabunge, viongozi mbalimbali wa kitaifa na itarushwa mbashara katika kituo cha radio na televisheni ya taifa ya TBC.

Taarifa hiyo imetolewa rasmi leo Juni 1, 2018 na kitengo cha Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

 

Video: Dkt. Hellen Kijo-Bisimba akanusha kuteuliwa baraza la wazee Chadema
Makala: Je unautumiaje urembo wako?