Kesi dhidi ya mtoto wa kiume Thabang Moswane (24), aliyemuua mama yake kisha kunywa damu yake imedaiwa kucheleweshwa kutokana na kutofikiwa kwa uamuzi wa iwapo shauri hilo lipelekwe Mahakama Kuu.

Kesi hiyo ambayo kwasasa ipo katika Mahakama ya Koster ya jimbo la Kaskazini Magharibi nchini Afrika Kusini, iliahirishwa kwa mara nyingine baada ya kesi dhidi ya mshtakiwa, uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, juu ya kuhamishia kesi hiyo katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Kaskazini Magharibi.

Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka imesema awali kesi hiyo iliahirishwa Julai 7, 2022 kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Mahakama kupokea taarifa za uchunguzi wa marehemu Kedisaletse Elizbeth Moswane (53), ambaye aliuawa na mwanaye.

Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka ya kikanda (NPA), Henry Mamothame amesema ripoti ya uchunguzi wa marehemu tayari imekamilika na kwamba kinachosubiriwa ni picha za tukio ambazo bado zinafanyiwa kazi ili uchunguzi ukamilike.

Thabang Moswane, anadaiwa kugombana na mama yake Kedisaletses Mei 9, 2022 katika ugomvi uliohusisha mambo ya pesa, baada ya kijana huyo mamake pesa taslimu kiasi cha Randi 10 na alipokataa, Moswane alimdunga kisu mamake hadi kumuua kisha kuanza kunywa damu yake iliyokuwa ikivuja katika majeraha.

Gazeti la Daily Sun la nchini humo, iliripoti kwamba kaka yake ambaye ni pacha wa Moswane, Thabo Moswane alimkuta mtuhumiwa akinywa damu ya mama yake katika jeraha la kisu alilomkata shingoni ambapo baadaye aliwaita Polisi wa Boons huko Mathopestad.

“Walipofika katika eneo la tukio, Polisi walipata mwili wa Kedisaletse ndani ya kibanda, ukiwa na majeraha mengi ya visu na wakamkamata mara moja na kisha siku chache baadaye wakamfikisha mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Koster.

Kijana huyo, Thabang Moswane sasa atarudishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Koster Septemba 1, 2022 ili kusikiliza mashitaka yanayomkabili.

MCT yatoa tathmini uhuru wa vyombo vya Habari nchini
Mabalozi watakiwa kuainisha fursa za kuinufaisha Tanzania