Usikilizwaji wa kesi kutoka pande zote za utetezi na mashtaka wa shauri la Polisi wa zamani wa Jiji la Minneapolis, Derek Chauvin, ambaye anashtakiwa kwa mauaji ya Mmarekani mweusi, George Floyd, unaanza leo Machi 29.

Watu 12 wanaounda Baraza la Mahakama wanatarajia kusikiliza ushuhuda katika kesi hiyo inayotarajiwa kuchukuwa mwezi mzima kukamilika.

Aidha Afisa huyo wa Polisi ambaye ni mzungu amepinga mashtaka yote yanayomkabili yanayohusu mauaji ya mwanaume mweusi, George Floyd akisema alichokifanya kiliendana na mafunzo ya kipolisi aliyopewa wakati alipokuwa akimkamata Floyd.

Floyd ambaye ni Mmarekani mweusi aliuawa kwa Chauvin kumbana kwa kutumia goti shingoni, karibu dakika tisa mwezi Mei mwaka 2020,

Waliomuua Mtangazaji wa ITV wasakwa
Mjumbe NEC: Magufuli alipambania Taifa bila kujali afya yake