Mahakama Kuu imepanga kusikiliza kesi ya wabunge wa viti maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliopinga uamuzi wa kuvuliwa uanachama wa chama hicho ambapo kesi hiyo itasikilizwa July 29, 2022, mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.

Mdee na wenzake walifungua kesi Mahakamani hapo kupinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA kuwavua uanachama wa Chadema Uliotolewa Mei 11, mwaka huu.

Wabunge hao wameiomba Mahakama itengue mchakato na uamuzi wa kuwavua uanachama, iwalazimishe CHADEMA kuwapa haki ya kuwasikiliza na amri ya zuio dhidi ya Spika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutohukua hatua yoyote mpaka malalamiko yao yatakapo amuliwa na Mahakama.

Hata hivyo, Uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA ulitokana na rufaa walizokata Mdee na wenzake baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa awali wa kamati kuu ya Chadema ya kuwavua Uanachama Novemba 27, 2022, kwa kile kilichodaiwa kuwatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu bila ridhaa ya chama.

Pia, walidai mchakato na uamuzi wa kuwafukuza uanachama haukuzingatia matakwa ya kisheria na misingi ya haki kwa kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa.

Uhuru agoma kumkabidhi Ruto nchi
Duchu aibukia Manungu-Turiani Morogoro