Kesi inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake imezidi kupigwa tarehe mara baada ya wakili wa Serikali, Hellen Moshi kusema kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Aidha, katika kesi hiyo washtakiwa hao ambao ni Harry Kitilya, Sioi Solomoni na Shose Sinare kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dolla za Marekani 550 millioni kwa Serikali ya Tanzania kutoka benki ya Standard ya Uingereza.

Hata hivyo, washtakiwa hao wanadaiwa kula njama za kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu ili waweze kujinufaisha wenyewe na washirika wao,

Muhimbili kuboresha maslahi ya wauguzi
Shirika la viwango Tanzania kuzalisha bidhaa zenye ubora