Kesi inayowakabili viongozi wakuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa imeahirishwa tena hadi Agosti 11, ili kupisha upepelezi zaidi.

Viongozi hao wakiwa pamoja na  Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Nsiande Isawafo Mwanga wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa mara ya nne na kusomewa mashitaka yao 28.

Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbroad Mashauri, amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa kwa sababu upelelezi haujakamilika na washtakiwa wanarudishwa rumande hadi Agosti 11 kesi hiyo itakapotajwa tena.

 Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga walipelekwa rumande Juni 29 baada ya kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam.
Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake pamoja na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga.
 Hata hivyo, Kesi zinazowakabili viongozi wa klabu ya Simba, Rais Evans Elieza Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ nayo imeahirishwa hadi  Agosti 7, mwaka huu kwa sababu pia upelelezi haujakamilika.

Mpina awang'ata sikio wananchi wa Kisesa
Gwajima atakiwa mahakamani Agosti 30