Mkoa wa Kagera umeadhimisha kilele cha wiki ya Sheria, huku Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Bukoba chini ya Jaji Mfawidhi Lameck M. Mlacha imeweza kusikiliza kwa mara ya kwanza kesi Namba 56 ya mwaka 2018 ya Mwalimu Respikius Patrick Mtazangira na Mwalimu Erieth Gerald dhidi ya mauaji ya Mwanafunzi, Spelius Eradius wa Kibeta Shule ya Msingi Manispaa ya Bukoba aliyepigwa hadi kupelekea kifo chake tarehe 27.08.2018
 
Katika shauri hilo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili, Chema Maswi Kaimu Mwendesha Mashitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo aliwasilisha mashahidi saba kutoa ushahidi katika shauri hilo.
 
Baada ya kutoa ushahidi huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Lameck M. Mlacha aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 8.02.2019 ambapo mashahidi wengine sita wataendelea kutoa ushahidi wao mbele ya Mahakama.
 
Aidha, kabla ya kikao hicho cha Mahakama Kuu, Jaji Mfawidhi Lameck M. Mlacha amesema kuwa maana ya kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya Sheria kwanza ni kiashiria cha kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama, Pili ni kuomba dua ili haki itendeke kwa wananchi Mahakamani, na tatu ni kufanya tathimini ya utendajikazi wa Mahakama kwa kipindi kilichopita na kujisahihisha.
 
  • Bomu aliloficha bwana harusi lamuua yeye na mpambe wake
 
  • Je, mifuko ya sare za polisi ni kishawishi cha kula rushwa?
 
  • Daladala zatakiwa kupisha ujenzi wa miundombinu kituo cha Gerezani
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti akitoa salamu za Serikali katika hafla hiyo aliipongeza Mahakama kwa kudumisha utamaduni wa kuadhimisha Wiki ya Sheria tena kwa kutoa msaada wa kisheria na elimu kwa wananchi na baadhi ya makundi mbalimbali ili yaweze kuelewa vizuri namna ya kutafuta haki Mahakamani

Bunge lamjadili Lissu kusimamisha mshahara wake
Bomu aliloficha bwana harusi lamuua yeye na mpambe wake