Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa Rushwa na Uhujumu Uchumi leo septemba 15 itaanza kupokea ushahidi wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeaman Mbowe na wenzake watatu.

Mashahidi wanaotarajiwa kutoa ushahidi Mahakamani hapo ni pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai.

Mashahidi wengine wanaotarajiwa kutoa ushahidi ni maofisa wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na wengine kutoka mikoani.

Wengine ni maaskari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akiwamo Luteni Denis Leo Urio kutoka Kikosi cha Jeshi cha Makomandoo, 92 KJ Ngerengere, mkoani Morogoro.

Pia wamo maofisa wa sheria kutoka kampuni za huduma za simu za mkononi za Mic Tanzania Ltd (Tigo) na Airtel.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mbowe, Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.

Young Africans kuondoka ijumaa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 15, 2021