Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu imeahirishwa mara tatu na Jaji Joachim Tiganga leo Novemba 17, 2021 kwa sababu tofauti tofauti ikwemo kuruhusu mawakili wa pande zote mbili kujadiliana.

Hata hivyo Jaji Tiganga ameahirisha kesi hiyo kwa muda kwa ajili ya kukagua kilichomo kwenye diary aliyokutwa nayo shahidi wa Jamhuri kizimbani.

Jaji Tiganga alilazimika kuahirisha kesi hiyo kwa mara ya pili ili kuruhusu majadiliano na mawakili wa pande zote juu ya maudhui waliyoyaona kwenye diary hiyo.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea mara baada ya majadiliano matatu kukamilika.

Dkt. Mpango ashiriki jukwaa la majadialiano ya kiuchumi
Ndayiragije: Gaita Gold ishinde kila mchezo kwa timu ipi?