Kesi ya mauaji dhidi ya mtoto wa kiume wa mwanasiasa maarufu nchini Nigeria, Bilyaminu Haliru Bello imeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu nchini humo.

Mke wa marehemu, Maryam Sanda anatajwa kama mtuhumiwa wa kwanza akidaiwa kumchoma visu mumewe hadi kufa, Oktoba mwaka jana.

Wawili hao hadi sasa wana mtoto wa miezi kumi waliyempata miezi michache kabla ya tukio hilo la mauaji.

Kesi hiyo imeshika vichwa vya habari nchini Nigeria kwa sababu Bello alikuwa mtoto wa Mwenyekiti wa chama cha People’s Democratic Party (PDP).

Mwenyekiti huyo alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa za nchi hiyo kwa miongo kadhaa.

Kutokana na mashahidi kutokuwepo mahakamani wakati wa kesi hiyo jana, Mahakama Kuu imeahirisha kesi hiyo hadi Aprili 19 mwaka huu.

African Beauty ya Diamond, Ua jekundu la Wema vyazua gumzo mtandaoni
Video: Lowassa amshukia Mkapa, Maagizo 9 ya JPM kwa wafanyabiashara