Kesi ya unyang’anyi kwa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya pamoja na wenzake wawili, imeahirishwa hadi Julai 16, 2021 mara baada ya shahid wa upande wa jamhuri kupata dharura.

Wakili wa serikali kwenye kesi hiyo Trasila Gervas ameiambia mahakama mbele ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Salome Mshasha kuwa shahidi waliyempanga ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na dharura.

Aidha wakili huyo wa serikali Gervas aliomba kupangwa siku nyingine ili mashahidi hao waanze kutoa ushahidi wao na hakimu mkazi mkuu, Salome Mshasha alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 16, 2021.

Rage: Mchakato uchaguzi TFF uko sawa
KMC FC yaendelea kuiwinda Simba SC